Nov 23, 2020 13:16 UTC
  • Raisi: Haki za binadamu zinatumiwa kama wenzo wa kuzishinikiza nchi huru duniani

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Iran amesema kuwa Canada inakiuka haki za binadamu na ni kimbilio la mafisadi na wahalifu. Ameongeza kuwa nchi mbaimbali duniani zimetambua kwamba haki za binadamu zimetiwa siasa kali na kugeuzwa wenzo wa kuziweka chini ya mashinikizo nchi huru duniani.

Akizungumza leo katika kikao cha Baraza Kuu la Vyombo vya Mahakama vya Iran, Sayyid Ibrahim Raisi ameongeza kuwa, akthari ya nchi hazikuunga mkono azimio eti la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran lililowasilishwa na Canada; na kama kawaida Marekani na utawala wa Kizayuni na baadhi ya nchi za Magharibi ndizo tu zilizoliunga mkono.  

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Iran ameeleza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaheshimu kikamilifu suala la kulinda haki za binadamu kwa maana yake halisi na kwa mujibu wa mafundisho ya dini; na kuongeza kuwa: Canada ambayo ni kimbilio la mafisadi, wezi, waporaji na wahalifu, yenyewe inapaswa kupitisha azimio kupinga suala hilo. 

Vikosi vya usalama vya Iran katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya katika mipaka ya nchi 

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Iran ameashiria namna Umoja wa Mataifa ulivyo na misimamo inayokinzana juu ya namna Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inavyoendesha vita dhidi ya madawa ya kulevya na wafanyamagendo na kueleza kuwa: Ulaya yote na Marekani zingeathiriwa na madawa ya kulevya iwapo Iran isingetekeleza jukumu lake la kudhibiti mihadarati.

Mkuu wa Vyombo vya Mahakamavya Iran aidha amepongeza maadhimisho ya Wiki ya Basiji na kueleza kuwa, adui hatoacha kulikodolea jicho la tamaa taifa hili la Kiislamu na tutaweza kuyashinda matatizo, njama na fitna zote za maadui, madhali Basiji ipo na ari yake inatawala humu nchini.

Tags