Nov 26, 2020 11:44 UTC
  • Rais Rouhani: Iran inaweza kuyadhaminia mataifa ya dunia mahitaji yao kwa bei rahisi zaidi

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehraninao uwezo wa kulidhaminia eneo hili na hata dunia nishati ya bei rahisi zaidi

Rais Rouhani amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa mirati ya taifa ya Wizara ya Mafuta ambao umefanyika kwa njia ya video.

Amesema kuwa, Iran imethibitisha kivitendo kuwa uchumi wake ni uchumi mkubwa na unaoweza kuhimili misukosuko mikubwa na kwamba katika eneo hili, hapana nchi yoyote yenye uwezo na nguvu za kupigana vita vikubwa vya vya kiuchumi kwa muda wa miaka mitatu mfululizo na kuweza kusimama kidete na kushinda.

Uchumi wa kimuqawama

 

Aidha amesema, taifa la Iran kwa kutegemea utamaduni wake, mara zote limekuwa likifanya kazi kubwa za kupigiwa mfano.

Vile vile amesema, katika upoande wa kijiografia na kijeopolitiki pia, Iran nchi muhimu ambayo dola lolote la dunia haliwezi kufuta ushawishi na umuhimu wake, si katika eneo hili tu, bali pia dunia nzima.

Leo Alkhamisi, Novemba 26, 2020, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezindua miradi mitatu mikubwa ya kitaifa ya Wizara ya Mafuta katika mikoa ya Bushehr, Chaharmahal va Bakhtiari na Khuzistan.

Itakumbukwa kuwa kwa miaka kadhaa sasa Marekani imeanzisha vita vikubwa vya kiuchumi na kimatibabu mbali na vita vyake vya zaidi ya miaka 40 dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, lakini taifa hili la Kiislamu limeendelea kubakia imara na kukabiliana vilivyo na njama zote hizo za maadui.

Tags