Nov 28, 2020 11:47 UTC
  • Rais Rouhani: Taifa la Iran litalipiza kisasi cha kuuliwa kigaidi, shahid Fakhrizadeh

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, maadui wote watambue kwamba, wananchi na viongozi wa Iran ni mashujaa na wenye ghera kubwa, hivyo lazima watalipiza kisasi cha vitendo vya jinai linavyofanyiwa taifa hili la Kiislamu.

Rais Hassan Rouhani amesema hayo leo Jumamosi katika kikao cha Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Ugonjwa wa Corona ikiwa ni kuonesha hisia zake baada ya maadui kumuua kigaidi mwanasayansi mkubwa wa Iran, Mohsen Fakhrizadeh na kusisitiza kukwa, ugaidi huo wa kinyama umeonesha kwamba maadui wa Iran ya Kiislamu wanapitia wiki nzito sana, wiki ambayo wanahisi hali duniani inazidi kubadilika dhidi yao na kwao wao ni muhimu sana kutumia wiki chache zilizobakia kutenda jinai kubwa kadiri wanavyoweza.

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kufuatia kuuawa shahid Dk Mohsen Fakhrizadeh

 

 

Kabla ya hapo pia Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa, maadui woga wa taifa wa Iran wajue kwamba kumuua shahidi Mohsen Fakhrizadeh hakutateteresha hata kidogo irada ya vijana na wanasayansi wa Iran ya Kiislamu ya kushikamana na njia ya ustawi wa kasi wa kielimu na kufikia kwenye vilele vya mafanikio ya kujivunia; lakini badala yake yatawafanya wawe na azma thabiti zaidi ya kuendeleza njia ya shahidi huyo mwenye hadhi kubwa; na damu za mashahidi wa Iran zitaendelea kubakia zikichemka na kutiririka.

Mohsen Fakhrizadeh, Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu la Wizara ya Ulinzi ya Iran aliuawa shahidi jana jioni katika shambulio la kigaidi lililofanywa katika viunga vya jiji la Tehran.

Mbali na masuala ya nyuklia na ulinzi, shahid Fakhrizadeh alikuwa mstari wa mbele pia katika kupambana na ugonjwa wa corona kiasi kwamba, kifaa cha kwanza kabisa cha kuchukulia vipimo vya COVID-19 nchini Iran kilibuniwa na kuundwa na taasisi aliyokuwa akiiongoza yeye.

Tags