Dec 01, 2020 12:53 UTC
  • Shirika la Atomiki la Iran latakiwa kuzalisha urani iliyorutubishwa kwa zaidi ya asilimia 20

Wabunge wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) wamelitaka Shirika la Atomiki la Iran kuzalisha urani iliyorutubishwa kwa zaidi ya asilimi 20 kwa ajili ya matumizi ya amani.

Katika kikao cha leo bungeni, wabunge wameafiki muswada wa 'mpango wa kistratijia wa kukabiliana na vikwazo na kulinda maslahi ya taifa'.

Kwa mujibu wa kipengee cha kwanza,  punde baada ya kupitishwa muswada huo, Shirika la Atomiki la Iran litawajibika kurutubisha madini ya urani kwa kiwngo cha zaidi ya asilimia 20 kwa ajili ya matumizi ya amani. Kiwango hicho cha urani iliyorutbishwa kwa zaidi ya asilimia 20 kinapaswa kuzidi kilo 120 kwa mwaka na urani hiyo iliyorutubishwa ibakishwe ndani ya nchi.

Aidha wabunge wa Iran wameafiki kipengee cha pili cha mswada huo ambacho kinashurutisha Shirika la Atomiki la Iran kurutubisha kilo 500 za madini ya urani kwa ajili ya matumizi ya amani na madini hayo pia yahifadhiwe ndani ya nchi. Kipengee cha tatu cha muswada huo kimeilitaka Shirika la Atomiki la Iran kuanza oparesheni ya kuanza kutumia kizazi cha tatu cha mashinepewa aina ya IR-2m na za kizazi cha sita aina ya IR-6.

Vipengee vyote vya muswada huo vikipitishwa, Iran itasitisha kwa muda majukumu zaidi ambayo ilikuwa imeahidi kuyatekeleza katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA ya mwaka 2015.

Bunge la Iran

Akizungumza katika kikao cha bunge, Abolfazl Amoeei, msemaji wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Bunge la Iran amesema muswada huo unalenga kuondoa vizingiti vyote vilivyokuwa vimewekwa katika mpango wa nyuklia wa Iran ili kufikia malengo ya juu ya mashahidi wa sekta ya nyuklia nchini kama vile Mohsen Fakhrizadeh, ambaye aliuawa shahidi Ijumaa katika oparesheni iliyotekelezwa na magaidi wanaofungamana na utawala haramu wa Israel.

Marekani ilijiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran ya JCPOA mwaka 2015 na kuanza kutekeleza vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

 

Tags