Dec 01, 2020 13:00 UTC
  • Rouhani: Adui ameghadhibika baada ya kushindwa kuangamiza uchumi wa Iran

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kusambaratika 'mashinikizo ya juu zaidi' ya Marekani dhidi ya Iran na kusema adui ameghadhibika baada ya kushindwa kufikia lengo lake la kuangamiza uchumi wa Iran.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo katika kikao cha Idara ya Serikali ya Kuratibu Uchumi na kuongeza kuwa, hata kama vikwazo vimesababisha matatizo na kuathiri vibaya uchumi na maisha ya wananchi, lakini adui ameshindwa kufikia lengo lake kuu la kuangamiza uchumi wa Iran kupitia vikwazo na vita vya kiuchumi. Rais Rouhani ameendelea kusema Iran imefanikiwa kukabiliana na vikwazo na kwamba mafanikio hayo makubwa yamepatikana kutokana na muqawama na kusimama kidete taifa la Iran pamoja na sera zenye busara.

Bandari ya Bandar Abbas kusini mwa Iran

Aidha amewahakikishia wananchi kuwa, uchumi wa kimapambano umeweza kufanikiwa na hivyo wenye kuwaza vikwazo hawana budi ila kuachana na sera yao hiyo na kwa msingi huo utabiri kuhusu mustakablia ni chanya.

Rais Rouhani amesema bajeti ya mwaka ujao wa 1400 Hijria Shamsia itajikita katika masuala ya ustawi na maendelo ya miundo msingi ya nchi.

Halikadhalika amesema bajeti ya mwaka ujao haitategemea pato la mafuta  ili kuweza kukabiliana na  vikwazo.

Tags