Dec 02, 2020 11:10 UTC
  • Rais Rouhani: Marekani haina budi kusalimu amri mbele ya muqawama wa taifa la Iran

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kushindwa 'siasa za Marekani za mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa' ni jambo ambalo linaifanya serikali mpya ijayo nchini humo isiwe na budi ila kusalimu amri mbele ya muqawama na kusimama kidete taifa hili la Kiislamu.

Rais Rouhani amesema hayo leo katika kikao na baraza lake la mawaziri ambapo amebainisha kwamba, serikali ya Marekani kuanzia mwaka 2018 imeshindwa vibaya kwani kila muswada dhidi ya Iran iliouwasilisha katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa haikufanikiwa kufikia malengo yake.

Dakta Hassan Rouhani amesema, katika miaka ya hivi karibuni Iran imekuwa na nguvu za kisiasa kiasi kwamba, wakati mwingine Marekani haikupata kura zaidi ya moja au mbili katika Baraza la Usalama katika njama zake dhidi ya Iran na  hata nguvu zote kubwa duniani kama Umoja wa Ulaya, Russia na China zilipinga miswada ya Washington dhidi ya Tehran.

Joe Biden, Rais mteule wa Marekani

 

Rais Rouhani amesema, katika upande wa masuala ya kisheria pia, shtaka la Iran dhidi ya Marekani katika Mahakama ya Kimataifa katika hatua ya awali lillikuwa na mafanikio ambapo hivi sasa pia lipo katika hatua nzuri na kuna matumaini ya kufanikiwa pia katika hatua za mwisho.

Kadhalika amesema kuwa, katika mazingira ya sasa nguvu za kiulinzi za Iran zimeimarika kuliko wakati mwingine wowote ambapo hivi sasa nguvu za kiulinzi za taifa hili ikilinganishwa na miaka minane iliyopita hususan katika silaha za kistratejia za baharni, chini ya bahari, manowari za kivita anga, helikopta za kijeshi, makombora na kadhalika kuna tofauti kubwa mno ambapo haiwezi kulinganishwa na wakati ule.

Tags