Dec 28, 2020 12:22 UTC
  • Khatibzadeh: Mizozo ya Afghanistan inaweza kupatiwa ufumbuzi kwa njia za kisiasa

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njia ya kuipatia ufumbuzi mizozo na mivutano inayoikabili Afghanistan ni utatuzi wa kisiasa.

Saeed Khatibzadeh amesema hayo leo katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari ambao umefanyika kwa mawasiliano ya Intaneti ambapo ameshiria mazungumzo ya juma lililopita ya Hamdullah Mohib, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Afghanistan na Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliyofanyika hapa mjini Tehran na kueleza kwamba, ufumbuzi usio na shaka wa migogoro na mizozo inayoikabili nchi hiyo ni wa kisiasa.

Aidha amesema kuwa, kwa kuzingatia uwepo wa Marekani nchini Afghanistan ambao unaharatisha amani na uthabiti wa nchi hiyo, Tehran inayataka makundi na pande zote za nchi hiyo kushiriki katika mazungumzo yanayozishiriki pande zote.

Hamdullah Mohib, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Afghanistan

 

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia pia kikao cha juma lililopita cha Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi zilizobakia katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kubainisha kwamba, Dakta Zarif alisisitiza katika kikao hicho juu ya upande wa pili kutekeleza ahadi zake kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Kadhalika amesema kuwa, hatua ya Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassim Suleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH lilikuwa kosa kubwa la kistratejia na kwamba, bila shaka waliotenda jinai hiyo kubwa ndani ya serikali ya Marekani watafikiwa na mkono wa uadilifu.

Tags