Jan 11, 2021 12:12 UTC
  • Khatibzadeh: Iran haiwezi kuwa mateka wa mashinikizo bandia ya watu walioshindwa

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran ikiwa serikali husika katika fremu ya ufundi na uchukuaji maamuzi kwa kujitegemea ndio inayopaswa kutoa majibu ya tukio la kuanguka ndege ya Ukraine katika anga ya taifa hili na kwamba, katu haitakubali kuwa mateka wa siasa na mashinikizo ya bandia ya pande zilizoshindwa.

Saeed Khatizadeh amesema hayo leo katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari  ambapo akizungumzia kadhia ya kuanguka ndege ya Ukraine amesema: Hatua za kimahakama za watuhumiwa wa tukio hilo ziko katika mkondo wake na hilo linafuatiliwa kwa nguvu zote. 

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema pia kuwa, Troika ya Ulaya inayoundwa na nchi za Uingereza, Ujerumani na Ufaransa haijatekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na hivyo madola hayo ni washirika wa Marekani katika uhalifu wake na kukiuka makubaliano hayo.

 

Kuhusiana na taarifa ya Troika ya Ulaya kuhusu mpango wa serikali ya Iran wa kurutubisha madini ya urani kwa kiwango cha asilimia 20, Khatibzadeh amesema kuwa, madola hayo si tu kwamba, yenyewe hayajatekeleza vyema majukumu yao bali yamekuwa washirika wa utawala wa Marekani katika kuyakiuka makubaliano hayo.

Aidha amesema kuwa, madola ya Troika ya Ulaya yanafahamu vyema  na kuliko taifa lolote lile kwamba, hatua ya Tehran ya kupunguza ahadi zake kwa mujibu wa JCPOA imezichukua katika fremu ya makubaliano hayo na kwa mujibu wa vipengee nambari 26 na 36 vya makubaliano hayo ya kimataifa.

Tags