Jan 25, 2021 23:40 UTC
  • Zarif: Safari yangu ya Azerbaijan ni mwanzo wa safari ya kieneo katika Ukanda wa Caucasia

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza mwishoni mwa safari yake mjini Baku Azerbaijan kwamba, katika safari yake ya Russia, Armenia, Georgia na Uturuki atafanya mazungumzo na viongozi wa nchi hizo kuhusiana na ushirikiano wa pande sita na ushirikiano mwingine wa kieneo.

Dakta Muhammad Javad Zarif alisema hayo jana Jumatatu wakati akibainisha matunda ya safari yake katika Jamhuri ya Azerbaijan ambapo aliwaambia waandishi wa habari kwamba, safari yake katika mji mkuu wa nchi hiyo Baku ni mwanzo wa safari ndefu ya kieneo katika eneo la Caucasia ambayo lengo lake ni kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi za eneo hilo kwa minajili ya kuimarisha mikakati ya amani na uthabiti katika eneo na vilevile kustawisha zaidi uhusiano wa pande mbili.

Dakta Zarif sambamba na kueleza kuwa, katika miezi ya hivi karibuni, Jamhuri ya Kiislamu ya iiran imekuwa na ushirikiano mzuri sana na Azerbaijan amebainisha kwamba, kumekuweko na safari za pande mbili za viongozi wa ngazi za juu kwa ajili ya kuyapatia ufumbuzi matatizo ya kieneo kama ambavyo kumefanyika juhudi pia za kufuatilia masuala yanayozihusu pande mbili.

Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

 

Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jumapili ya juzi aliwasili Baku mjini Mkuu wa Azerbaijan akiuongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Tehran.

Baada ya Azerbaijan, Dakta Zarif anatarajiwa kuzitembelea pia Russia, Armenia, Geogia na Uturuki, safari ambayo inatajwa na duru za habari kuwa ina umuhimu wa aina yake.