Jan 30, 2021 12:20 UTC
  • Rouhani: Taifa la Iran lilisambaratisha udikteta na ubeberu

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Taifa la Iran kwa mapambanao na muqawama limeweza kusambaratisha ubeberu."

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo Jumamosi ambapo ametoa pongezi kwa mnasaba wa kuanza Alfajiri 10 za Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: "Taifa moja, kwa muqawama na mshikamano, lilifanikiwa kusambaratisha ubeberu na udikteta na hivyo kumtimua Shah, Marekani na mabeberu wengine kutoka Iran."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni tukio lisilo na kifani katika historia na kuongeza kuwa, baada ya maelfu ya miaka utawala uliochakaa wa kifalme uliangushwa na badala yake ikaja madarakani serikali ya demokrasia ya kidini.

Imam Khomeini-Mwenyezi Mungu Amrehemu-  akiwahutubia wananchi baada ya kurejea kutoka uhamishaoni

Ikumbukwe kuwa 12 Bahman mwaka 1357 Hijria Shamsia sawa na Februari Mosi 1979,  Imam Khomeini (MA) Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, alirejea nchini na kupokelewa kwa shangwe kubwa na wananchi baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka kadhaa. Mapokezi hayo makubwa ya wananchi wa Iran kwa Imam Khomeini hayajawahi kushuhudiwa mfano wake katika historia ya sasa ya dunia. 

Siku kumi baada ya kurejea nchini Imam,  yaani Februaria 11 1979, Mapinduzi ya Kiislamu yalipata ushindi kamili. Kipindi hicho cha siku kumi za baina ya kurejea Imam nchini hadi kupata ushindi kamili Mapinduzi ya Kiislamu, kinajulikana hapa nchini kama "Alfajiri Kumi". Kila mwaka hufanyika sherehe kubwa kwa mnasaba wa kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Tags