Apr 12, 2021 10:35 UTC
  • Saeed Khatibzadeh
    Saeed Khatibzadeh

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran italipiza kisasi kwa wakati mwafaka kutokana na uharibifu uliofanywa na Israel katika kituo cha nyuklia ya Natanz.

Saeed Khatibzadeh amewaambia waandishi habari hii leo Jumatatu mjini Tehran kwamba, uharibifu uliofanywa na Israel katika kituo cha nyuklia cha Natanz haupunguzi uwezo wa nyuklia wa Iran na kuongeza kuwa: Kilichokuwepo huko Natanz ni mashenepewa za kizazi cha kwanza ambazo zinabadilishwa na kuwekwa mashine za kisasa zaidi. Amesisitiza kuwa kilichofanyika huko Natanz hakiwezi kurejesha nyuma sekta ya kuzalisha nishati ya nyuklia ya Iran wala hakitakuwa na taathira katika jitihada za kuondoa vikwazo.

Kuhusu namna Iran itakavyolifuatilia tukio hilo la Natanz kisheria na kisiasa, Khatibzaded amesema: Iran ina haki ya kujihami kwa mujibu wa kifungu nambari 51 chati ya hati ya Umoja wa Mataifa na kitendo hiki ni ugaidi wa kinyuklia ambao ungeweza kusababisha maafa ya binadamu; hivyo kinaorodheshwa katika safu ya jinaii dhidi ya binadamu.

Kuhusu kimya cha Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) mkabala wa kitendo hiicho cha Israel huko Natanz, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: IAEA na mashirika mengine ya kimataifa yalipaswa kulaani kitendo hicho na kufanya jitihada za kuzuia kukakariwa kwake. 

Msemaji wa Shirika la Atomiki la Iran, Behrouz Kamalvandi amesema kuwa, mapema jana Jumapili kulishuhudiia tukio katika sehemu moja ya mtandao wa kusambaza umeme katika kituo cha kurutubisha madini ya uranium cha Shahid Ahmadi Roshan huko Natanz. 

Behrouz Kamalvandi 

Kamalvandi amesema sababu ya tukio hilo bado inachunguzwa na taarifa kamili itatolewa hapo baadaye.