Apr 14, 2021 03:17 UTC
  • Iran yaanza operesheni ya kuzalisha urani iliyorutubishwa kwa asilimia 60

Msemaji wa Shirika la Atomiki la Iran amestangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu imeutumia barua Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ikiujulisha kuwa inaanza operesheni ya kuzalisha madini ya urani yaliyorutubishwa kwa asilimia 60.

Behrouz Kamalvzandi amesema maandalizi ya kuanza uzalishaji huo yalifanyika jana usiku katika Kituo cha Kurutubisha Madini ya Urani cha Ahmadi Roshan huko Natanz hapa nchini.

Kamalvandi amesema: Kutokana na amri iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Shirika la Atomiki linalazimika kuanza operesheni ya uzalishaji wa urani iliyorutubishwa kwa asilimia 60 kwa kadiri ya mahitaji ya nchi, katika fremu ya kifungu nambari moja cha Sheria ya Hatua ya Kistratijia ya Kufuta Vikwazo na Kulinda Maslahi ya Taifa la Iran iliyopasishwa na Bunge. 

Amesema barua ya kuanza mipango ya uzalishaji wa urani iliyorutushwa kwa asili 60 imekabidhiwa kwa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia, na hatua za utekelezaji ilianza mara moja jana usiku.

Msemaji wa Shirika la Atomiki la Iran ameongeza kuwa, urani iliyorutubishwa kwa asilimiai 60 inatumika katika uzalishaji wa elementi za molybdenum zinazotumiwa katika uundaji wa aina balimbali za dawa za nyuklia za radiopharmaceutical. Amesema mashinepewa mpya za IR1 zinachukua nafasi ya mashine za zamani katika urutubishaji huo.   

Tags