Apr 16, 2021 12:08 UTC
  • Saeed Namaki
    Saeed Namaki

Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran imezidisha kasi katika utengenezaji wa chanjo ya kukabiliana na virusi vya corona.

Saeed Namaki amesema kuwa, kazi ya kutengeneza chanjo ya corona hapa nchini inafanyika kwa kasi kubwa. 

Namaki amesema kazi ya kutengeneza chanjo hiyo hapa nchini imefikia kiwango kizuri sana na kuongeza kuwa: Katika mustakbali si wa mbali nchi zenye miundombinu bora ya masuala ya afya ndizo zitakazoweza kutoa chanjo kwa raia wao.

Waziri wa Afya wa Iran amesema kuwa, karibu chanjo laki tano za virusi vya corona zimetolewa nchini hadi leo na kwamba, hadi mwishoni mwa wiki ijayo chanjo milioni moja na laki tatu za kukabiliana na virusi vya corora zitakuwa zimetolewa hapa nchini.

Saeed Namaki amewapongeza na kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa jitihada zao kubwa katika kipindi hiki cha maambukizi ya corona. 

Mbali na kuagiza chanjo ya corona kutoka nje, wasomi na wataalamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wanatengeneza chanjo kadhaa za kukabiliana na vifrusi vya corona, suala ambalo limepongezwa na duru za kisayansi na kielimu duniani.

Iran inafanyia majaribio chanjo kadhaa za kukabiliana na corona

Ni vyema kukumbusha hapa kuwa, Iran iko mbioni kuunda chanjo kadhaa za Covid-19, ambapo mbali na  chanjo ya COVIran Barekat, chanjo zingine ambazo zimepiga hatua nzuri katika majaribio ni pamoja na Razi Cov Pars,  Fakhra na chanjo ya pamoja ya Taasisi ya Chanjo ya Finlay ya Cuba na Taasisi ya Chanjo ya Pasteur ya Iran.   

Tags