Apr 22, 2021 07:53 UTC
  • IAEA yathibitisha: Iran imeanza kufunga mashinepewa za kisasa Natanz

Vyombo vya habari vya Marekani mapema leo Alkhamisi vimewanukuu maafisa wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) wakithibitisha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeutaarifu wakala huo kwamba itafunga mashinepewa za kisasa katika taasisi ya kurutubisha madini ya urani ya Natanz.

mwandishi wa gazeti la Wasll Street Journal mjini Brussels amewanukuu maafisa wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki kwkamba Iran imewasilisha rasmi mipango yake ya kusimika mashinepewa za kisasa aina ya IR-4 katika taasisi ya kurutubisha madini ya urani ya Natanz.  

Wiki iliyipita msemaji wa Shirika la Atomiki la Iran alitangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu imeutumia barua Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ikiujulisha kuwa inaanza operesheni ya kuzalisha madini ya urani yaliyorutubishwa kwa asilimia 60.

Kamalvandi amesema: Kutokana na amri iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Shirika la Atomiki linalazimika kuanza operesheni ya uzalishaji wa urani iliyorutubishwa kwa asilimia 60 kwa kadiri ya mahitaji ya nchi, katika fremu ya kifungu nambari moja cha Sheria ya Hatua ya Kistratijia ya Kufuta Vikwazo na Kulinda Maslahi ya Taifa la Iran iliyopasishwa na Bunge. 

Amesema barua ya kuanza mipango ya uzalishaji wa urani iliyorutushwa kwa asili 60 imekabidhiwa kwa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia, na hatua za utekelezaji ilianza mara moja jana usiku.

Kamalvandi

Msemaji wa Shirika la Atomiki la Iran ameongeza kuwa, urani iliyorutubishwa kwa asilimiai 60 inatumika katika uzalishaji wa elementi za molybdenum zinazotumiwa katika uundaji wa aina balimbali za dawa za nyuklia za radiopharmaceutical. 

Hivi karibuni pia Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisisitiza kuwa urutubishaji wa madini ya urani kwa kiwango cha asilimia 60 ni jibu kwa vitendo vya shari vya maadui.

Rais wa Iran alikuwa akishiria tukio la hivi karibuni la uharibifu uliofanywa katika kituo cha nyuklia cha Natanz katikati mwa Iran siku chache zilizopita. Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran italipiza kisasi kwa wakati mwafaka kutokana na uharibifu uliofanywa na Israel katika kituo hicho cha Natanz.