Apr 23, 2021 02:31 UTC
  • Mwanachuo wa kike wa Iran atunukiwa tuzo katika Shindano la Ubinifu Afrika

Mwanafunzi wa kike wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametunukiwa medali mbili tofauti katika Shindano la Ubunifu Afrika la mwaka huu 2021.

Hayo yalitangazwa jana Alkhamisi na Amir-Abbas Koushki, Mkuu wa Timu ya Ubunifu ya Iran ambaye ameeleza kuwa, mwanachuo huyo wa kike wa Kiirani, Mobina Ghazi ametuzwa medali moja ya fedha na moja ya shaba kutokana na kazi zake za ubunifu alizoziwasilisha kwenye shindano hilo.

Koushki amesema Ghazi amepewa tuzo ya shaba kutokana na mradi wa "Hospitali Erevu" aliouwasilisha kwenye shindano hilo la Africa Innovation Challenge 2021. Ameongeza kuwa, binti huyo Muirani pia ametuzwa nishani ya fedha kwa mradi wa pili wa "Roboti-erevu ya kukabiliana na Corona."

Mkuu wa Timu ya Ubunifu ya Iran kadhalika amesema wavumbuzi wa Iran wametunukiwa tuzo ya fedha katika Mashindano ya kimatiafa ya uvumbuzi na ubunifu ARCA ambayo hufanyika mjini Croatia kila mwaka katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Croatia katika mji wa Zagreb. 

Wanachuo wa kike wa Iran wana nafasi kubwa katika masuala ya ubunifu na uvumbuzi

Shindano hilo la Ubinifu Afrika 2021 limefanyika wakati huu ambapo dunia inakwenda mbio kubuni na kuvumbua vifaa na suhula za kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.

Ikumbukwe kuwa, Novemba mwaka 2019, timu ya Iran ambayo ilivumbua 'glovu erevu ya kielektroniki yenye joto' ilifanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya kimataifa ya uvumbuzi na ubunifu nchini Croatia.

Tags