May 05, 2021 11:53 UTC
  • Rais Rouhani: Iran imesambaratisha vikwazo

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vikwazo dhidi ya nchi hii vimesambaratishwa.

Rais Rouhani ameyasema hayo katika kikao cha baraza la mawaziri na kuongeza kuwa: "Upande wa pili unafahamu kuwa hauna njia nyingine ghairi ya kurejea katika sheria na ahadi zake katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameendelea kusema kuwa: "Leo ni siku ya maombolezo kwa Wazayuni ambao kupitia Marekani walianzisha vita vya kiuchumi dhidi ya Iran."

Ameongeza kuwa Wazayuni wamegonga mwamba katika vita hivyo na pia katika njama zao za kuitenganisha Iran na nchi za eneo .

Rais Rouhani amesema njia ya kufika ukingoni vikwazo iko wazi na kwamba haki za taifa la Iran lazima zizingatiwe kikamilifu katika mapatano ya JCPOA. Aidha amesema Iran haitafumbia macho haki zake zote.

Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu

Kwingineko katika hotuba yake, Rais Rouhani ameashiria siku ya Kimataifa ya Quds na kusema: "Wiki hii tuna Siku ya Quds. Hii ni siku ambayo ni fakhari kwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ni kati ya wosia wa Imam Khomeini (MA).

Rais Rouhani ameongeza kuwa: "Taifa la Palestina litarejea katika ardhi zake na mji wa Quds, pamoja na Msikiti wa Al Aqsa, qibla cha kwanza cha Waislamu, vitarejea kwa Waislamu."

Tags