May 09, 2021 02:15 UTC
  • Kamanda Salami: Tutamzika adui katika kaburi la historia

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amesema kuwa, Tehran haitaruhusu maadui kuharibu matunda na mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu na kwamba, adui atazikwa akiwa dhalili na hakiri katika kaburi la historia.

Meja Jenerali Hussein Salami ambaye alikuwa akizungumza kwa mnasaba wa kuwakumbusha mashahidi wa Harakati ya Walinzi wa Haram waliouawa katika eneo la Khan Tuman huko Syria wakipambana na magaidi wa kundi la Daesh na wabwana zao, amesema kuwa maadui wamepatwa na mfadhaiko, kufeli na kushindwa, na kuongeza kuwa, Uislamu unaendelea kuenea zaidi kutokana na kusimama kidete, subira, ushujaa na kujitoa mhanga kwa mashahidi.

Meja Jenerali Salami amesema kuwa, japokuwa mashahidi wamepata muradi na maratajio yao kwa kupata daraja ya juu ya kuuliwa shahidi, lakini familia zao hazikufikia matarajio yao kutokana na kuwaaga watoto wao waliouliwa shahidi, na jambo hili linahitajia uvumilivu, kujitolea na imani kubwa. 

Meja Jenerali Hussein Salami

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amepongeza moyo wa kujisabilia, kusimama imara na uvumilivu wa familia za mashahidi na kusema: "Tutaendelea kubeba bendera ya kuulinda Uislamu ya mshahidii hao hadi mwisho wa uhai wetu na hatutaruhusu matunda yao yavurugwe na kuharibiwa." 

Eneo la Khan Tuman liko Kusini Magharibi mwa Aleppo nchini Syria. Tarehe 5 Mei mwaka 2016 kundi la vijana wa Harakati ya Walinzi wa Haram na kaburi ya Mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), Bibi Zainab huko Syria waliuawa shahidi katika mapambano makali yaliyotokea eneo hilo la Khan Tuman.

Tags