May 12, 2021 09:57 UTC

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei alasiri ya jana alihutubia mkutano wa wawakilishi wa jumuiya na asasi za wanachuo nchini uliofanyika kwa njia ya intaneti na kuelezea masikitiko yake makubwa kutokana na matukio mawili machungu mno ya umwagaji damu yaliyotokea karibuni katika Ulimwengu wa Kiislamu, huko Afghanistan na Palestina na kulaani jinai zilizofanyika katika nchi hizo.

Akiashiria jinai za kutisha na za kinyama za Wazayuni huko Masjidul Aqsa, Quds tukufu na maeneo mengine ya Palestina, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amepongeza mwamko, kusimama kidete na azma kubwa ya Taifa la Palestina na kuongeza kuwa: Wazayuni hawaelewi sipokuwa lugha ya mabavu, hivyo Wapalestina wanapaswa kuongeza nguvu na mapambano yao ili wawalazimishe watenda jinai hao wasalimu amri na kusimamisha hatua zao za kinyama.

Kwa zaidi ya wiki mbili sasa mji wa Quds na Msikiti wa al Aqsa vimeshuhudia mashambulizi ya wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakiwahujumu Waislamu waliokuwa wakitekeleza ibada ya Swala ndani ya Msikiti wa al Aqsa na raia wengine wa Palestina. Hali mbaya ya Quds, Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza iliyosababishwa na tabia ya Wazayuni maghasibu ya kuendelea kuuvunjia heshima Msikiti wa al Aqsa na kibla cha kwanza cha Waislamu imewalazimisha wanamapambano wa Palestina kuvurumisha makombora kadhaa dhidi ya vitongoji vya walowezi kandokando ya Gaza wakijibu jinai na hujuma hizo. Wapalestina hawakutosheka na jibu hilo, bali harakati ya Jihad Islami pia imeulenga mji mkuu wa utawala huo haramu, Tel Aviv na miji mingine ya Israel kwa maroketi kadhaa.

Wanaharakati wa Palestina wamevuirumusha makombora kadhaa dhidi ya Israel

Jinai na uhalifu wa Wazayuni dhidi ya taifa liinalodhulumiwa la Palestina na kukaririwa mashambulizi ya kigaidi huko Afghanistan baada ya hujuma iiliyolenga shule ya wasichana ya Sayyidu Suhada katika viunga vya Kabul, vyote vinatokana na chimbuko na chanzo kimoja. Ukweli ni kuwa, chanzo na chimbuko la matatizo mengi ya Ulimwengu wa Kiislamu kuanzia ugaidi hadi mauaji ya kinyama dhidi ya wanawake na watoto wadogo huko Afghanistan, Palestina na Yemen na kulazimishwa mamilioni ya wanawake na watoto kuwa wakimbizi, ni matokeo ya siasa na sera za kijuba na kupenda makuu, uvamizi na himaya ya madola makubwa ya kibeberu kwa madhalimu na watendajinai. Ni kwa kutilia maanani ukweli huo ndipo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akasisitiza masuala mawili katika hotuba yake ya jana:

Kwanza ni sisitizo lake kuhusiana na masuala ya kibinamu katika kadhia ya Palestina. Taifa la Palestina limekuwa mhanga wa dhulma ya kihistoria na licha ya kupita zaidi ya miongo 7 sasa tangu ardhi ya Palestina ivamiwe na kukaliwa kwa mabavu na Wazayuni, lakini dunia ingali inaangalia kwa macho tu jinai za utawala huo haramu bila ya kuchukua hatua yoyote ya maana.

Ayatullah Ali Khamenei ameshiria ukweli huo mchungu na kusema: "Jinai hizi zinafanywa mbele ya macho ya walimwengu; kwa hivyo watu wote wanapaswa kuzilaani na kila mmoja atekeleze wajibu wake.

Image Caption

Suala jingine lililosisitizwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika hotuba yake ya jana ni udharura wa kuendelezwa mapambano kama njia pekee ya kurejesha haki zilizoporwa za taifa la Palestina. Ayatullah Khamenei alisisitiza kuwa, ukombozi wa Palestina hautapatikana ila kwa kusimama kidete na mapambano ya kishujaa. Amesema: "Taifa, wanaharakati na jumuiya za Kipalestina zinapaswa kuibana Marekani na adui Mzayuni kwa Jihadi na kujitolea, na Umma mzima wa Kiislamu unalazimika kuunga mkono na kusaidia mapambano hayo ya kishujaa."

Taifa la Palestina kwa sasa limeimarika zaidi na limeazimia kukomboa ardhi yake kutoka kwenye makucha ya wazayuni maghasibu. Kiongozi wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), Ismail Hania anasema: Hamas imeazimia ipasayo kukabiliana na maghasibu hadi utawala huo utakapositisha kikamilifu ugaidi wake huko Quds na katika Msikiti wa al Aqsa. 

Ismail Hania

Vilevile Majid Safataj ambaye ni mchambuzi wa masuala ya siasa anasema: Uzoefu wa miongo saba ya dhulma ya kihistoria dhidi ya taifa la Palestina unaonesha kuwa, Wavamizi wa Kizayuni kamwe hawatatoa haki za taifa linalodhulumiwa la Palestina. Hivyo, njia pekee ya kukomesha hali hii ni kuendeleza mapambano ya kuwalazimisha Wazayuni maghasibu wasalimu amri mbele ya sheria za kimataifa na kukubali pendekezo la kuwapa Wapalestina haki ya kujiainishia mambo.  

Tags