May 14, 2021 03:31 UTC
  • Hossein Amir-Abdollahian: muqawama wa Palestina utavuruga mahesabu kwa namna ya kushtua

Msaidizi Maalum wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, katika awamu mpya muqawama wa Palestina utavuruga mahesabu kwa namna ya kushtukiza na kushangaza.

Hossein Amir-Abdollahian amesema hayo katika ujumbe wake wa Twitter ambapo ameandika:  Kama Wazayuni hawatasimamisha hujuma na mashambulio yao dhidi ya Ukanda wa Gaza, basi katika awamu mpya muqawama wa Palestina utavuruga mahesabu kwa namna ya kushtukiza na kushangaza.

Ukatili wa wanajeshi wa Israel umeongezeka sana katika mwezi wa Ramadhani wa mwaka huu, na utawala wa Kizayuni umefanya jinai dhidi ya Waislamu wa Palestina na Kibla cha Kwanza cha Waislamu kiasi kwamba hata watu wasio Waislamu wanaendelea kulaani jinai hizo.

Utawala wa Kizayuni umeendeleza jinai zake dhidi ya wananchi wa kawaida wa Palestina na hadi hivi sasa umeshaua makumi ya raia wasio na hatia.

Wanajeshi Wazayuni wakiangalia kwa hofu athari za mashambulio ya wanamapambano wa Kisilamu wa Palestina

 

Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, wananchi  zaidi ya 72 wa Palestina wameshauawa shahidi kutokana na mashambulizi ya kikatili ya Wazayuni ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo watoto 17 ni miongoni mwa Wapalestina waliouawa shahidi hadi hivi sasa, 388 kati yao wamejeruhiwa, 115 kati ya hao waliojeruhiwa katika mashambulio ya kikatili ya Wazayuni ni watoto wadogo na 50 ni wanawake. 

Ripoti zinasenma kuwa, wanamuqawama wa Palestina wameshayapiga kwa makombora zaidi ya  540 maeneo mbalimbali ya kiuchumi ya Israel katika kipindi cha siku nne zilizopita na kuusababishia utawala huo katili hasara ya dola milioni 160.

Tags