May 18, 2021 13:47 UTC
  • Wabunge wa Iran wataka kufutwa vikwazo vyote ilivyowekewa Tehran

Wabunge 200 wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) wametoa tamko la pamoja la kutaka kufutwa vikwazo vyote ilivyowekewa Iran.

Kwa mujibu wa Iran Press, zaidi ya wabunge 200 wa Iran wamesema katika taarifa yao hiyo ya pamoja kwamba siasa zisizotetereka za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kufutwa vikwazo vote  na baada ya Tehran kufanya uchunguzi na kujiridhishwa kuwa ni kweli vikwazo hivyo vimefutwa ndipo nayo itarejea kutekeleza kikamilifu ahadi zake ndani ya mapambano ya nyuklia ya JCPOA.

Katika taarifa yao hiyo wabunge hao wamesema, Bunge la Iran halitambui tofauti wala mgawanyo wowote ambao walioweka vikwazo hivyo wanajaribu kuuaminisha ulimwenguni. Bali Bunge linavihesabu vikwazo vyote kuwa ni sawa sawa, hakuna tofauti yoyote baina yao.

Vikwazo

 

Wabunge wa Iran pia wamesisitiza katika taarifa yao hiyo kwamba, kama vikwazo vyote havitaondolewa kwa asilimia mia moja, basi itakuwa ni kama vile hakuna kikwazo chochote kilichoondolewa.

Tamko hilo limeongeza kuwa, Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) itatumia sheria ya hatua ya kiistratijia kwa ajili ya kuhakikisha vikwazo vyote vinafutwa na manufaa ya taifa la Iran yanalindwa, kama ambavyo pia itaendelea kusimamia kwa kina utekelezaji wa mchakato huo.

Wabunge wa Iran vile vile wamesema, tunahimiza na kutilia mkazo kulindwa kikamilifu mafanikio waliyopata wataalamu wa nchi yetu katika sekta ya nyuklia. Tunatilia mkazo jambo hilo katika kalibu ya "Sheria ya Hatua ya Kiistratijia ya Kufuta Vikwazo."

Tags