May 27, 2021 11:22 UTC
  • Amir Abdolahian: Siri ya ushindi wa matawalia wa kambi ya muqawama, ni umoja

Msaidizi Maalumu wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amesisitiza kuwa, siri ya ushindi wa mfululizo wa kambi ya muqawama ni umoja na mshikamano wake.

Hossein Amir Abdollahian amesema hayo katika mahojiano na tovuti ya habari ya al Ahd ya Lebanon kwa mnasaba wa maadhimisho ya kila mwaka ya ukombozi wa kusini mwa Lebanon.

Amegusia ushindi wa hivi karibuni wa wanamuqawama wa Palestina dhidi ya utawala wa Kizayuni katika vita vya "Upanga wa Quds" vilivyopiganwa kwa muda wa siku 12 kwa ajili ya kuihami Quds Tukufu na Msikiti wa al Aqsa na kusisitiza kuwa, umoja na mashikamano ndiyo silaha kuu iliyowapa ushindi wanamuqawama wa Palestina.

Ameongeza kuwa, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan pamoja na Ukanda wa Ghaza, maeneo yote hayo mawili ya Wapalestina yametoa watu waliokufa shahidi katika kuilinda Quds na Msikiti wa al Aqsa.

Makomandoo wa Hizbullah ya Lebanon

 

Amesema, ushindi wa wanamapambano wa Palestina katika vita vya hivi karibuni vya siku 12 pamoja na ushindi mwingine wa kambi ya muqawama katika maeneo mbalimali umepatikana chini ya kivuli cha umoja na mshikamano. Amesema, mlingano wa dhahabu nchini Lebanon yaani ushirikiano wa pande tatu; jeshi, wananchi na muqawama ndio ulioliletea ushindi mkubwa taifa la Lebanon na ndio unaoisaidia nchi hiyo kuvuka salama katika migogoro mbalimbali.

Msaidizi Maalumu wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa pia amesema, viongozi wa utawala wa Kizayuni muda mrefu walikuwa wanatuma watu wa kupatanisha ili wawaokoe kutoka kwenye kinamasi walichokuwa wamekwama huko kusini mwa Lebanon.

Tags