Jun 13, 2021 11:35 UTC
  • Rais Rouhani
    Rais Rouhani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, njia ya kutayarisha, kutengeneza na kutoa chanjo ya corona tayari imeandaliwa.

Akizungumza katika kikao cha 232 cha Kamati ya Serikali ya Uratibu wa Kiuchumi, Rais Hassan Rouhani ameeleza kuwa: Hatua zinazotekelezwa na serikali na hiyama yake kwa chanjo zinazozalishwa hapa nchini ni mipango ya uhakika na ya siku za usoni katika mkondo sahihi, na kwamba njia ya kutayarisha, kutengeneza na kutoa chanjo tayari imeandaliwa.   

Utoaji chanjo nchini Iran umeandaliwa kikamilifu 

Rais Rouhani ameongeza kuwa,  serikali imeshughulikia suala la ununua mapema chanjo za corona zinazotengenezwa hapa nchini, na hatua za lazima zimeshachukuliwa.  

Rais wa Iran ameongeza kuwa, Benki Kuu imejaribu imefanya jitihada kubwa za kudhamini na kutoa fedha za kigeni zinazohitajika kwa wafanyabiashara wa pembejeo za mifugo licha ya vikwazo vya kidhalimu ilivyowekwa na madola ya kibeberu dhidi ya nchi hii vinavyotatiza suala la kupatikana fedha za kigeni. 

Suala la kutayarisha fedha kwa ajili ya kununua chanjo za corona zinazozalishwa ndani ya nchi imejadili na kuchunguzwa katika kikao hicho cha Rais wa Iran na Kamati ya Serikali ya Uratibu wa Masuala ya Kiuchumi.