Jun 14, 2021 12:59 UTC
  • Jeshi la Majini la Iran lapata meli mbili mpya za kivita zilizoundwa nchini

Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo limepokea meli mbili mpya za kivita ambazo zimeundwa kikamilifu hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa, manoari mbili ambazo ni meli ya kisasa ya kivita iliyopewa jina la Dena na meli ya kuondoa mabomu yaliyotegwa baharini iliyopewa jina la Shahin zimezinduliwa leo katika mji wa pwani wa Bandar Abbas kusini mwa Iran. Manoari hizo zimekabidhiwa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika shererehe ambayo imehutubiwa kwa njia ya video na Rais Hassan Rouhani. Katika hotuba yake, Rais Rouhani amesema majeshi ya Iran yameweza kujitosheleza kwa kutegemea uwezo wa ndani ya nchi.

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Amir Hatami akizungumza katika hafla hiyo amesema manoari hizo mbili zilizozinduliwa zimeundwa kikamilifu nchini Iran na kuongeza kuwa meli ya kivita ya Dena inaweza kuenda kwa kasi kubwa na ina uwezo wa oparesheni mbali baharaini.

Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Amir Hatam

Huku akiashirai kuwa Iran ina pwani yenye masafa ya kilomita 2,500 amesema ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa nchi za eneo na dunia ni ujumbe wa amani na urafiki na kuongeza kuwa Iran imeweza kuthibitisha kuwa ni mshirika mwenye kuaminika.

Tags