Jun 16, 2021 12:27 UTC
  • Wagombea 2 wajiondoa katika kinya'nganyiro cha urais nchini Iran

Wagombea wawili kati ya saba wa Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unaotazamiwa kufanyika katika kipindi cha siku mbili zijazo wametangaza kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.

Wawili hao ni Alireza Zakani na Mohsen Mehralizadeh. Wagombea waliosalia katika kinyang'anyiro hicho cha Ijumaa ijayo ni pamoja na Saeed Jalili, Mohsen Rezaee Mirgha'ed, Sayyid Ebrahim Raisi,  Sayyid Amir-Hossein Ghazizadeh Hashemi, na Abdolnaser Hemmati.

Uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya kesho kutwa ya tarehe 18 mwezi huu wa Juni, ndani na nje ya nchi. 

Rais wa sasa Hassan Rouhani anayemaliza muhula wake wa pili mfululizo haruhusiwi kugombea urais katika awamu hii.

Wananchi wa Iran wanasubiri kwa hamu na shauku kuu kushiriki zoezi hilo la kidemokrasia

Katika hatua nyingine, Msemaji wa Makao Makuu ya Uchaguzi wa Rais hapa nchini amesema matokeo ya urais yatangaza katika kipindi kifupi baada ya kufungwa vituo vya kupigia kura.

Esmaeil Mousavi amesema, "Tumepanga tutangaza matokea ya Uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufikia adhuhuri siku ya Jumamosi."

Tags