Jun 18, 2021 03:24 UTC
  • Uchunguzi wa maoni: Raeis anaongoza kwa kuwa na zaidi ya asilimia 68 ya kura

Uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni unaonyesha kuwa mgombea urais Ebrahim Raeisi utashinda kwa kupata asilimi 68.9 ya kura.

Utafiti huo uliokamilishwa Alkhamisi (Juni 16) - siku moja tu kabla ya uchaguzi, umeonyesha kuwa asilimia 8.1 ya watu watakaoshiriki kwenye uchaguzi wa leo watampigia kura Mohsen Rezaei.

Mgombea wa mrengo wa mageuzi Abdul Nasser Hemmati alikuwa akishika nafasi ya tatu kwa kuwa na asilimia 4.6 akifuatiwa na Amir-Hossein Ghazizadeh-Hashemi.

Asilimia 14.6 ya wapigakura walikuwa bado hawajaamua watampa nani kura zao.

Wagombea watatu wa urais, ambao ni Mohsen Mehr-Alizadeh, Alireza Zakani, na Saeed Jalili, walijiondoka kwenye kinyang'anyiro hicho Jumatano iliyopita.

Jana Alkhamisi Rais anayemaliza muda wake wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Dakta Hassan Rouhani kwa mara nyingine alitoa mwito kwa wananchi wa Iran kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi akisisitiza kuwa, kwa kushiriki vilivyo katika uchaguzi, taifa la Iran halitoruhusu kuaguka ndoto za adui.

Rais Hassan Rouhani ameeleza hayo leo Alkhamisi na kuongeza kuwa; maadui wanataka kuona uchaguzi wa Iran unakuwa baridi na akasema kuhudhuria kwa wingi wananchi katika masanduku ya kupigia kura kutakwamisha kufikiwa ndoto za adui.

Tags