Jun 21, 2021 10:27 UTC
  • Rais Hassan Rouhani
    Rais Hassan Rouhani

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, magaidi wa Kimarekani wamekiri kikamilifu kwamba wamewafungia Wairani kila kitu zikiwemo shughuli zinazohusiana na masuala ya benki.

Rais Rouhani ambaye mapema leo amezindua miradi kadhaa ya maendeleo katika eneo la biashara huru la Aras huko kaskazini magharibi mwa Iran amtoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa mjukuu wa Mtume Muhammad (saw), Imam Ali bin Mussa Ridha (as) na akasema: Licha ya mashaka mengi waliyokumbana nayo katika vita vya kiuchumi visivyo na mfano katika historia ya Mashariki ya Kati, wananchi wa Iran wamesimama kidete katika vita hivyo vya madhalimu wa White House ambao wameizingira Iran kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu. 

Rais Rouhani amesema kuwa, matamshi ya maafisa wa Wizara ya Fedha ya Marekani siku tatu zilizopita ambao walisema kuwa wako tayari kuiondolea vikwazo Iran katika masuala ya chanjo ya corona ni kukiri kwa magaidi hao kwamba, wamewafungia Wairani milango ya kila kitu zikiwemo shughuli za kibenki. Amesema Wamarekani wanadai kuwa wako tayari kuiondolea Iran vikwazo vinavyohusiana na barakoa na chanjo ya corona baada ya kujua kwamba, Iran haina haja na vitu hivyo kwa sababu inavizalisha yenyewe ndani ya nchi.

Rais Rouhani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu amesema kuzinduliwa kwa miradi ya maendeleo ya matrilioni ya fedha katika eneo la biashara huru la Aras ni ushahidi wa kufeli na kushindwa vita vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya taifa la Iran.