Jun 23, 2021 13:03 UTC
  • Iran yakosoa  hatua ya Marekani ya kufunga tovuti za IRIB

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekosoa hatua ya Marekani ya kufunga tovuti kadhaa za Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) na kusema hiyo ni njama ya kuvuruga uhuru wa moani.

Katika taarifa, Saeed Khatibzadeh, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema hatua ya Marekani kufunga tovuti kadhaa zilizo chini ya IRIB ni katika njama ya Washington ya kuzima sauti huru katika vyombo vya habari duniani.

Khatibzadeh, amesema hatua hiyo ni muendelezo wa undumakuwili wa sera za Marekani na kuongeza kuwa, serikali ya sasa ya Marekani inafuata ule ule mkondo wa Marekani na sera hizo hazitakuwa na natija nyingine ghairi ya kugonga mwamba.

Hali kadhalika amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itafuatilia kisheria hatua hiyo ya Marekani ya kufunga tovuti za Iran.

Saeed Khatibzadeh, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Jana serikali mpya ya Marekani ilifunga tovuti za televisheni za kimataifa za IRIB ambazo ni Press TV, Al Alam na Al Khauthar. Kufuatia hatua hiyo Press TV imetangaza kuwa tovuti iliyofungwa ya presstv.com sasa inapatikana kupitia presstv.ir