Jul 14, 2021 04:06 UTC
  • Mishkini: Magharibi ikomeshe sera za undumakuwili mkabala na ugaidi

Msemaji wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesisitiza kuwa, nchi za Magharibi zinapasa kukomesha mienendo yake ya undumakuwili kuhusiana na ugaidi.

Mahmoud Abbaszadeh Mishkini amesem, nchi za Magharibi zinadai kupambana na ugaidi na wakati huo huo zinaliunga mkono kundi la kigaidila Munafiqin (MKO). Mishkini ameashiria utambulisho halisi wa kundi la kigaidi la MKO na kuongeza kuwa, utambulisho wa kundi hilo uko wazi kwa walimwengu. Amesema MKO ni kati ya magaidi ambao mikono yao illijaa damu ya wananchi wa Iran katika kipindi cha mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini kwa sababu zaidi ya Wairani elfu 17 wameuawa na wanachama wa kundi hilo la kigaidi.  

Viongozi wa nchiza Magharibi akiwemo John Bolton pamoja na kiongozi wa Munafiqin 

Msemaji wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje katika Bunge la Iran ameongeza kuwa, kundi la kigaidi la MKO lilikuwa pamoja na chama cha Baath cha Iraq dhidi ya wananchi wa Iran wakati wa vita vya kulazimishwa vya Saddam Hussein dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.  

Abbaszadeh Mishkini amesema, Marekani na nchi za Magharibi kwa ujumla zinapiga nara za kutetea haki za binadamu na kupambana na ugaidi lakini katika kipindi chote cha miaka 40 iliyopita nchi hizo zimeasisi makundi ya kigaidi ili kupambana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; jambo linalokinzana na nara na shaari zao. 

 Amesisitiza kuwa, nchi za Magharibi zinawafadhili kifedha na  kuwapatia silaha magaidi na kundi la MKO na kwamba jambo hilo ni kielelezo cha kufeli pakubwa siasa za Wamagharibi.  

Tags