Jul 24, 2021 08:08 UTC
  • Marais wa Tanzania na Kenya wamtumia salamu za pongezi Rais mteule wa Iran

Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kenya wamemtumia ujumbe Ayatullah Ibrahim Raesi wakimpongeza kwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa mwezi uliopita wa Rais hapa nchini.

Katika ujumbe wake mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sambamba na kumpongeza Sayyid Ibrahim Raesi rais mteule wa Iran kwa ushindi alioupata katika uchaguzi uliopita amesema kuwa, ushindi huo ni ishara ya wazi imani walionayo wananchi kwake.

Rais wa Tanzania amesema pia kuwa, serikali yake ya awamu ya sita itaendeleza himaya, uungaji mkono na ushirikiano wake na Jamhuri ya Kiislamu ya  Iran.

Mama Samia Suluhu Hassan amesisitiza pia kwamba, serikali yake itashirikiana na Ayatullah Raeisi, serikali yake ijayo na wananchi wa Iran kwa ujumla kwa ajili ya kupanua zaidi ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali.

Ayatullah Sayyid Ibrahim Raeisi, Rais mteule wa Iran

 

Wakati huo ho, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya naye amemtumia ujumbe wa pongezi Sayyid Ibrahim Raiesi na kusisitiza kwamba ,uhusiano wa Tehran na Nairobi umekuwa imara na madhubuti katika miaka yote hii na kwamba, mwenendo wa ushirikiano huo utaendelea kwa misingi ya ushirikiano wa pande mbili na kuamianiana.

Kadhalika Rais Uhuru Kenyatta ameeleza kuwa, ana matumaini uhusiano na ushirikiano wa Iran na Kenya utapanuka na kuimarika zaidi katika kipindi cha urais wa Ayatullah Raeisi.

Sayyid Ebrahem Raeisi alitangazwa mshindi katika kinyang'anyiro hicho cha Juni 18 mwaka huu, kwa kupata kura karibu milioni 18 za wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Tags