Jul 27, 2021 11:54 UTC
  • Mazungumzo ya makamanda wa majeshi ya majini ya Iran na Russia; sisitizo la kuimarishwa ushirikiano wa baharini

Admeri Hossein Khanzadi kamanda wa kikosi cha majini cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo katika mji wa bandari wa Saint Petersburg na Nikolai Yevmenov, Kamanda wa kikosi cha majini cha Jeshi la Russia ambapo wawili hao wamejadili njia za kupanua ushirikiano wa baharini.

Udharura wa kuchukuliwa hatua za pamoja katika fremu ya kupanua ushirikiano wa pande zote katika uga wa kiulinzi na kiusalama, kufanyika manuva ya pamoja ya majini, kuongeza uwezo wa manowari za baharini za nchi mbili katika maeneo ya kistratijia duniani na kuwa na mitazamo ya pamoja kadiri inavyowezekana baina ya pande mbili kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vya pamoja ni miongoni mwa zilizokuwa ajenda kuu za mazungumzo ya makamanda wa vikosi vya majini vya Iran na Russia.

Mazungumzo hayo yamefanyika pambizoni mwa uwepo wa kikosi cha 77 cha Manowari za Iran katika manuva makubwa ya majini ya Russia kwa mnasaba wa maadhimisho ya miaka 325n ya kuasisiwa manowari ya nchi hiyo. Kamanda wa kikosi cha majini cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameshiriki katika sherehe kama mgeni maalumu.

Iran ndicho kikosi chenye nguvu zaidi miongoni mwa vikosi vya majini vilivyoshiriki katika manuva hayo ya majini ya Russia, ambapo Iran imeshirikki katika sherehe hiyo ikiwa na manowari mbili kubwa za Makran na Sahand. Kwa mtazamo wa wachambuzi wa mambo na vituo vya utafiti wa masuala ya kistratijia ni kuwa, ushirikiano wa kijeshi katika kiwango cha juu kama hiki, una maana maalumu.

Latika kutathmini uwezo wa kikosi cha majini cha jeshi la Iran, Kituo cha Kistratijia cha Tabyin sambamba na kuashiria kufanyika kwa manuva ya pamoja ya kijeshi ya Iran, Russia na China ya 27 Disemba 2019 kaskazini mwa Bahari ya Hindi na Bahari ya Oman kinabainisha kwamba:

Manowari ya Makran

 

Ushirikiano huu unaweza kutathminiwa kwa msingi ya nadharia ya 'kuangalia mambo kwa uhalisia wake katika kujilinda". Nadharia hii inaamini kwamba, katika mazingira ambayo nchi fulani inafanya hima ya kuyatisha mataifa mengine, mataifa hayo yanaweza kutoa majibu ya awali ya vitisho hivyo kwa kuongeza na kuimarisha uwezo wao wa kiulinzi. Miongoni mwa vitisho vinavyotolewa na Marekani katika eneo ambavyo tunaweza kuviashria ni uwepo mkubwa wa kijeshi wa Washington katika maeneo ya mipaka ya kijiografia ya Iran

Mazungumzo ya makamanda wa vikosi vua majini vya majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia katika kiwango hiki ni ishara ya wazi ya umuhimu wa ushirikiano wa kistratijia hususan katikka eneo la Asia Magharibi. Eneo la Asia Magharibi na Ghuba ya Uajemi daima yamekuwa na umuhimu maalumu kwa Marekani.

Kwa mujibu wa nadharia za wasomi kama Alfred Thayer Mahan aliyekuwa akisisitiza umuhimu wa kupelekwa jeshi katika eneo la Asia Magharibi, Marekani baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia daima ilifanya juhudi za kuyadhibiti maeneo mbalimbali ya eneo hili. Kwa mujibu wa misingi yake na mikakati huru katika sera zake za kigeni zilizojengeka juu ya msingi wa kupinga ubebeberu wa Marekani katika mfumo wa kimataifa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikisisitiza kuondoka haraka Marekani na madola mengine ya Magharibi katika eneo hili na imesema mara chungu nzima kwamba, usalama wa Asia Magharibi unapaswa kudhaminiwa na mataifa ya eneo hili.

Admeri Hossein Khanzadi kamanda wa kikosi cha majini cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran 

 

Uwezo wa kijeshi na kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambao leo umethibiti katika nyuga mbalimbali ni jambo ambalo limeyapa msukumo mataifa kama Russia wa kuitazama Iran kama mshirika wa kuaminika kwa ajili ya kulinda amani na uthabiti kwa kutegemea uwezo wa ndani wa eneo.

Kikosi cha jeshi la majini cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kina nafasi maalumu katika utengenezaji huu wa uwezo. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza siku nyingi utayari wake wa kushirikiana na majirani zake katika kudhamini amani na usalama wa Ghuba ya Uajemi na imewahi kupebndekeza mpango wa "Ubunifu wa Amani ya Hormoz".

Mkakati huo ambao umejengeka juu ya msingi wa ushirikiano wa pande kadhaa, unaainisha kujifunga Iran na suala la kulinda usalama wa njia muhimu za majini. Filihali manowari za kikosi cha majini cha kistratijia cha jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kinachoundwa na manowari za Kiirani za Sahand na Makran zipo katika maji ya kimataifa kwa lengo la kuonyesha uwezo wa kiulinzi na wa kumfanya adui ashindwe kuanzisha shambulio. Uwepo huu wenye nguvu ni ishara ya wazi ya nafasi muhimu na ya kistratijia iliyonayo Iran katika usalama jumla katika eneo.