Aug 04, 2021 12:14 UTC
  • Meja Jenerali Salami: Majibu yetu yatakuwa haribifu, ya kusambaratisha na ya kumfanya adui ajute

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) amezungumzia propaganda za vyombo vya habari vya maadui na kusema kuwa, maadui wanapaswa kutambua kwamba, majibu yetu yatakuwa haribifu, ya kusambaratisha na ya kuwafanya wajute.

Meja Jenerali Hossein Salami amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na kubainisha kwamba, kufuatia mafanikio ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, maadui wamefanya hima ya kutumia vibaya matukio yanayotokea hapa nchini kama vile matatizo ya uhaba wa maji, umeme na kadhalika kwa ajili ya kufikia malengo yao.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) amesisitiza kuwa, katika hatua ya ukabidhianaji madaraka, hapa nchini hili linatofautaina na ukabidhianaji madaraka huko nchini Marekani ambapo, hapa kwetu mwenendo huu wa kisiasa unafanyika kwa unyenyekevu, usalama na utulivu wa hali ya juu.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH)

 

Kamanda Salami ameeleza pia kuwa, maadui wamekuwa wakifanya njama za kupandikiza wasiwasi, hata hivyo tunawaonya maadui na kuwataka wajifunze kwa matukio ya huko nyuma.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) ameongeza kuwa, ni miaka 42 sasa ambapo taifa hili limekuwa likikabiliana na adui na hivi sasa liko imara, madhubuti na lenye idara yenye nguvu zaidi kuliko huko nyuma.

Meja Jenerali Salami amebainisha pia kuwa, maadui wanapaswa kufutilia mbali fikra zao batili kwani jibu la taifa hili kwa chokochoko za kwa taifa hili litakuwa haribifu, la kusambaratisha na la kumfanya adui ajute.