Aug 19, 2021 15:37 UTC
  • Swala ya Adhuhuri ya Ashura yaswaliwa kote katika Iran ya Kiislamu

Waombolezaji kote katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo wameswali Swala ya Adhuhuri ya Ashura katika kumbukumbu ya siku aliyouawa shahidi kiongozi wa mashahidi, Imam Hussein AS.

Kwa mujibu wa taarifa, leo waumini kote Iran wamejitokeza katika maeneo ya wazi na kwa kuzingatia kaununi za kiafya za kuzuia kuenea Corona ambapo kuanzia mapema asubuhi walishiriki katika hafla ya kumuomboleza Imam Hussein bin Ali AS. 

Baada ya adhana ya adhuhuri, waumini walishiriki katika swala ya jamaa kukumbuka namna Imam Hussein AS alivvoswali akiwa katika medani ya vita huko Karbala.

Hafla ya maombolezo katika mkesha wa Ashura katika moja ya maeneo ya Iran

Katika tukio la Karbala lililojiri katika siku kama ya leo mnamo mwaka 61 Hijria, Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib AS, Imamu wa Tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia duniani alisisitiza na kueleza bayana kwamba: "Kusudio langu ni kuufichua na kuufedhehesha utawala ulio dhidi ya Uislamu, kuamrisha mema na kukataza mabaya na kukabiliana na dhulma na uonevu."

Mafunzo ya harakati ya Imam Hussein AS yamesambaa na kutanda katika historia na jiografia ya viumbe, wanadamu na ulimwengu mzima na hayawezi katu kuishia kwenye mipaka maalumu.

Tags