Sep 11, 2021 06:59 UTC
  • Mwanasoka wa Iran akataa kuchezea klabu yake ya Uholanzi katika mechi ya kimataifa na timu ya Kizayuni

Klabu ya soka ya Feyenoord Rotterdam ya Uholanzi imekubali ombi la Alireza Jahanbakhsh mwanasoka wa timu ya taifa ya Iran anayechezea timu hiyo la kutoandamana nayo katika mechi dhidi ya timu ya Kizayuni ya Maccabi Haifa katika michuano ya klabu za Ulaya.

Shirika la habari la IRIB limeripoti kuwa, klabu ya Feyenoord ya Uholanzi imekubali ombi la Jahanbakhsh la kutoandamana nayo katika mechi dhidi ya timu ya Kizayuni ya Maccabi Haifa katika michuano ya klabu za Ulaya.

Jumanne ya wiki hii, timu ya Feyenoord inatazamiwa kupambana na timu ya Maccabi Haifa inayowakilisha utawala wa Kizayuni wa Israel katika michuano ya soka ya Europa Conference League. Mechi hiyo imepangwa kufanyika katika uwanja wa soka wa Haifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavuu, ambapo Alireza Jahanbakhsh, mwanasoka wa Iran anayechezea timu ya Feyenoord Rotterdom hataandamana na timu yake katika mechi hiyo.

Alireza Jahanbakhsh (mwenye mpira) 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Feyenoord Rotterdom, kocha wa timu hiyo amelikubali ombi la Jahanbakhsh la kutoandamana na klabu yake huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu, kwa sababu wanamichezo wa Kiirani siku zote huwa hawako tayari kupambana na wale wanaowakilisha utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.../

Tags