Sep 17, 2021 11:21 UTC
  • Russia yataka Iran iondolewe vikwazo vyote vya nyuklia ilivyowekewa

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika asasi za kimataifa zenye makao yake mjini Vienna Austria ametoa wito wa kuondolewa vikwazo vyote vya nyuklia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mikhail Ulyanov, mwanadiplomasia mwandamizi wa Russia ambaye pia ni mjumbe wa nchi yake katika mazungumzo ya nyuklia amesisitiza kuwa, kuna haja ya kuondolewa vikwazo vyote vya nyuklia.

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika asasi za kimataifa zenye makao yake mjini Vienna Austria amesisitiza kuwa, kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kuna mfungamano na kuondolewa vikwazo vikwazo vyote vya nyuklia ilivyowekewa Iran.

Hivi karibuni, Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema kuwa, Marekani imetoa pigo kuu kwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA; na si mtuhumiwa bali ndiye mhalifu mkuu katika ukiukaji wa makubaliano hayo.

 

Tarehe 8 Mei 2018 Marekani chini ya utawala wa Donald Trump, ilijitoa kwenye mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA na kuiwekea Iran vikwazo vikubwa zaidi ambavyo havijawahi kutokea. Ijapokuwa awali serikali ya Marekani wakati huo ilidai kuwa inataka mapatano ya nyuklia ya JCPOA yaangaliwe upya ndio maana imejitoa kwenye makubaliano hayo, lakini hivi sasa inatangaza waziwazi lengo lake hasa la kujitoa kwenye mapatano hayo.

Taifa la Iran limekabiliana na vikwazo vya kiwango cha juu vya Marekani kwa muqawama wa kiwango cha juu na kufelisha njama za serikali ya Washington.

Tags