Sep 19, 2021 07:54 UTC
  • Indhari ya Meja Jenerali Bagheri kwa makundi ya kigaidi yaliyo dhidi ya mapinduzi ya Kiislamu kaskazini mwa Iraq

Mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametahadharisha kuhusu chokochoko za makundi ya kigaidi na yaliyo dhidi ya mapinduzi ya Kiislamu kaskazini mwa Iraq.

Meja Jenerali Mohammad Bagheri ameashiria leo katika hafla ya kumuaga na kumuarifisha Naibu Mkuu wa majeshi ya Iran kuhusu oparesheni ya karibuni ya jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) huko kaskazini mwa Iraq na katika eneo la Kurdistan nchini humo na kueleza kuwa: Viongozi wa eneo hilo na serikali ya Iraq wanapasa kuchukua hatua kukabiliana na makundi hayo. 

Askari wa Sepah

Meja Jenerali Bagheri amewatahadharisha viongozi wa Marekani kwamba wanapasa kuvunja pia kambi zao zilizopo katika eneo hilo. Amesema Iran itaendelea kufanya oparesheni dhidi ya makundi yaliyo dhidi ya mapinduzi na haitavumilia uhabithi wowote katika mipaka ya maeneo hayo. 

Mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa ni haki ya Iran kukabiliana na makundi hayo ya kigaidi na kwamba hati ya Umoja wa Mataifa pia imezingatia haki hiyo ya Iran. 

Tags