Sep 19, 2021 16:34 UTC
  • Khatibzadeh: Kuna udharura wa kuundwa serikali jumuishi nchini Afghanistan

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, kuna udharura wa kuundwa serikali itakayoshirikisha makundi na kaumu zote za Afghanistan.

Saeed Khatibzadeh ambaye leo Jumapili alikuwa akizungumza na waandishi habari mjini Tehran amesema matokeo ya mazungumzo ya viongozi wa Jumuiya Ushirikiano ya Shanghai huko Dushanbe nchini Tajikistan yatatangazwa hivi karibuni.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameongeza kuwa, katika safari ya Dushanbe, Rais Ebrahim Raisi na Waziri wa Mashauri ya Kigeni Hussein Amir-Abdollahian walifanya mazungumzo na wenzao katika Jumuiya ya Ushirkiano wa Shanghai kuhusu kadhia ya Afghanistan na kwamba suala hilo lilikuwa moja ya ajenda kuu za mkutano huo. 

Katibzadeh amesema kuwa, Afghanistan inapaswa kuwa nchi yenye amani na isiyo na ugaidi na kuongeza kuwa, Waafghani wenyewe wanapaswa kuchukua maamuzi kuhusu mustakbali wa nchi yao bila ya kuingiliwa na madola ya kigeni. 

Tags