Sep 20, 2021 08:00 UTC
  • Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani
    Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani

Waziri wa Ulinzi wa Iran amejibu chokochoko na bwabwaja za viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel akisema kuwa Jeshi la Taifa la Iran litatoa jibu kali kwa hatua ya aina yoyote ya kijinga.

Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani ameyasema hayo leo kwenye mkutano wa wakurugenzi wa ngazi za juu wa Wizara ya Ulinzi akijibu madai yasiyo ya msingi na bwabwaja za maadui wa Jamhuri ya Kiislamu hususan baadhi ya viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kuongeza kuwa: Iran imetangaza mara kwa mara kwamba, uwezo wa kujihami wa taifa kubwa la Iran na maendeleo yake yanayotegemea teknolojia ya kisasa ni kwa ajili ya kulinda usalama na mipaka ya Jamhuri ya Kiislamu na kutoa jibu kali kwa vitisho vya aina yoyote vya adui.

Brigedia Jenerali Reza Ashtiani amesema taifa shupavu la Iran litaendelea kuwepo katika medani zote za mapambano dhidi ya maadui kwa moyo wake imara unaotokana na imani na ujasiiri. 

Waziri wa Ulinzi wa Iran ametoa onyo kali kwa maadui wa Jamhuri ya Kiislamu na kusema, mikono ya shetani na tawala tegemezi kwa madola ya kibeberu yameamua kutoa bwabwaja na tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Iran.

Akiashiria tuhuma zilizotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Brigedia Jenerali Reza Ashtiani amesema, utawala huo bandia ambao daima umekuwa ukipata vipigo na kushindwa mbele ya taifa la Iran umefeli na kushindwa pia katika fikra za walimwengu wa watetezi wa uhuru na hauwezi lolote isipokuwa kumalizia vinyongo na hasira zake kwa wanawake na watoto wanaodhulumiwa wa Palestina.