Sep 21, 2021 02:42 UTC
  • Eslami: Marekani inapasa kuondoa vikwazo vyote kivitendo dhidi ya Iran

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema kuwa wakati umefka kwa Marekani kurekebisha siasa zake ghalati, na katika hatua ya kwanza iondoe kivitendo vikwazo vyote, kwa njia athirifu na kutoa hakikisho.

Mohammad Eslami ambaye ni Makamu wa Rais na Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran alisisitiza jana katika Mkutano Mkuu wa 65  wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kwamba, kwa mujibu wa hati ya IAEA wakala huo una wajibu wa kuzisaidia bila ubaguzi nchi wanachama kustawisha na kustafidi na nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani. Ameongeza kuwa wakala wa IAEA unapasa kuzisaidia na kuwa bega kwa bega na nchi wanachama kufanikisha malengo endelevu ya nchi hizo kwa njia ya kuzipatia elimu, tajiriba, teknolojia na suhula mbalimbali bila ya ubaguzi wala kuingiza masuala ya siasa katika kadhia hiyo.  

Eslami amesema Iran inashirikiana na wakala wa IAEA na wakati huo huo kuna ulazima wakala huo pia ujiepusha na masula ya siasa katika utendaji wake. Amesema IAEA inapasa kulinda uhuru wake, kutoegemea upande wowote na kufanya kazi kwa mujibu wa taaluma.  

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema, mapatano ya nyuklia ya JCPOA yaliyofikiwa baina ya nchi za kundi la 5+1 na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa lengo la kuondoa vizuizi vya maendeleo ni mfano wa wazi wa nia njema ya Iran. Amesema, Marekani imekiuka vipengee vya mapatano hayo na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutokana na sera zake za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja na kujitoa katika mapatano hayo ya kimataifa. 

Rais wa wakati huo wa Marekani, Donald Trump alipotangaza kuitoa Marekani katika JCPOA 

 

Tags