Sep 21, 2021 13:26 UTC
  • Waziri wa Ulinzi wa Iran: Kamwe hatutoruhusu kufanikiwa njama za maadui

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kamwe hatutoruhusu njama za maadui zifanikiwe kukwamisha mustakbali wa nchi yetu.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo leo na kumnukuu  Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani akisema hayo na kuongeza kuwa, maadui wa Mapindzi ya Kiislamu wanaendesha njama za kubadilisha mtindo wa maisha wa Kiislamu - Kiirani katika jamii ya wananchi wa Iran hasa kupitia kufifiliza matukufu ya kidini na kimapinduzi kwa lengo la kuisambaratisha jamii hiyo ya Waislamu.

Waziri wa Ulinzi wa Iran ameongeza kuwa, jambo linalopaswa kupewa kipaumbele katika vita hivi vikali viivyojaa njama za kila namna za adui, ni kukuza na kubakisha hai matukufu ya kimapinduzi hususa ushujaa na kujitolea muhanga mashujaa wa Iran katika vita vya kujihami kutakatifu na haipasi kuruhusu njama potofu za maadui zikwamishe ujenzi wa mustakbali bora wa nchi yetu.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikituma satalaiti yake mwenyewe katika anga za mbali

 

Jana pia, Waziri wa Ulinzi wa Iran alijibu chokochoko na bwabwaja za viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel akisema kuwa Jeshi la Taifa la Iran litatoa jibu kali kwa hatua ya aina yoyote ya kijinga.

Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani alisema hayo kwenye mkutano wa wakurugenzi wa ngazi za juu wa Wizara ya Ulinzi akijibu madai yasiyo ya msingi na bwabwaja za maadui wa Jamhuri ya Kiislamu hususan baadhi ya viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kuongeza kuwa: Iran imetangaza mara kwa mara kwamba, uwezo wa kujihami wa taifa kubwa la Iran na maendeleo yake yanayotegemea teknolojia ya kisasa ni kwa ajili ya kulinda usalama na mipaka ya Jamhuri ya Kiislamu na kutoa jibu kali kwa vitisho vya aina yoyote vya adui.