Oct 13, 2021 08:00 UTC
  • Mkurugenzi Mkuu wa IAEA: Hujuma dhidi ya vituo vya nyuklia inapasa zilaaniwe

Katika kile kinachoelezewa kama msimamo uliochukuliwa kwa kuchelewa na wa kujitoa kimasomaso, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amesema, hujuma na shambulio lolote dhidi ya vituo vya nyuklia inapasa vilaaniwe.

Rafael Grossi ameyasema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na jarida la Energy Intelligence kuhusu mauaji ya kigaidi ya wanasayansi wa nyuklia wa Iran na hujuma zilizofanywa dhidi ya vituo vya atomiki vya Jamhuri ya Kiislamu.

Grossi ameeleza kuwa, mkutano mkuu wa IAEA ulipitisha maazimio kadhaa huko nyuma yaliyotoa msimamo wadhiha na wa uwazi kuhusu suala hilo na akaongeza kwamba, kwa mujibu wa maazimio hayo, shambulio lolote dhidi ya mitambo na vituo vya nyuklia inapasa lilaaniwe.

Baada ya hujuma na uharibifu uliofanywa kwenye kituo cha nyuklia cha Iran cha Natanz, Kazem Gharib Abadi, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu katika mashirika ya kimataifa yenye makao yao mjini Vienna alitangaza kuwa, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA ametakiwa atoe msimamo wa wazi kuhusu shambulio la Natanz, sambamba na kulaani shambulio hilo la kigaidi.

Shahidi Mohsen Fakhrizadeh

Kwa mujibu wa Hati ya IAEA, mbali na wakala huo wa kimataifa wa nishati ya atomiki kuwa na kazi ya usimamizi, una wajibu na jukumu pia la kutumia uwezo wake kulinda miradi ya nyuklia ya nchi wanachama na kila aina ya hujuma. Hata hivyo kuhusiana na Iran, wakala huo haukutekeleza jukumu lake hilo.

Ukweli ni kwamba IAEA na nchi wanachama wa wakala huo hazikuonyesha radiamali wala kuchukua yoyote kuhusiana na hujuma za kigaidi zilizofanywa dhidi ya Iran, zikiwemo za uharibifu katika kituo cha Natanz na mauaji ya mwanasayansi mkubwa wa nyuklia shahidi Mohsen Fakhrizadeh.../