Oct 14, 2021 02:20 UTC
  • Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh
    Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh

Kamanda wa Kikosi cha Anga na Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) amesema kuwa, mifumo yote ya kiulinzi iliyotumiwa katika luteka ya Walinzi wa Anga Velayat-1400 ni ya Kiirani.

Akizungumza pambizoni mwa luteka ya pamoja ya Walinzi wa Anga ya Velayat-1400, Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh ameongeza kuwa, katika luteka hiyo kufanyika vita dhidi ya adui vilivyoshirikisha makundi mawili moja la adui bandia na jeshi letu la ulinzi.  

Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh ameshiria ulinzi wa pande zote mkabala na mashambulizi makali ya ndege zisizo na rubani katika eneo la mazoezi hayo ya kijeshi na kueleza kuwa, katika luteka hiyo jeshi la Iran limefanikiwa kupiga maeneo mbalimbali na kulenga shabaha makombora ya Cruz kwa mafanikio. 

Kombora la Cruz 

Kamanda Hajizadeh amesema, katika luteka hiyo vikosi vya ulinzi va Iran vimetumia kwa mara ya kwanza mabomu yenye mabawa yanayoongozwa kutoka mbali kutoka kwenye ndege.