Oct 16, 2021 07:22 UTC
  • Iran yajibu madai ya rais wa Jamhuri ya Azerbaijan

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Iran ameyataja kuwa ya kustaajabisha na bandia madai mapya ya rais wa Jamhuri ya Azerbaijan dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kikao cha viongozi wa Jumuiya ya Madola ya Nchi Huru (CIS) na kusema Iran inakanusha vikali mada hayo.

Katika taarifa siku ya Ijumaa, Saeed Khatibzadeh, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria madai yaliyo dhidi ya Iran ya Ilham Aliyev  Rais wa Jamhuri ya Azerbaijan kuwa eti Iran inashirikiana na Armenia katika biashara ya mihadarati na kusema: "Kutoa tuhuma kama hizo katika vyombo vya habari kunafanyika kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unataka kuvuruga uhusiano wa kidugu baina ya mataifa mawili ya Iran na Jamhuri ya Azerbaijan.

Khatibzadeh amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya mihadarati na kuongeza kuwa, maelfu ya Wairani wameuawa shahidi na kujeruhiwa katika kipindi cha miongo minne wakikabiliana na mihadarati na hii ni sehemu tu ya jitihada endelevu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika njia hii. Aidha amesema taasisi za kimataifa zimethibitisha kuwa Iran iko mstari wa mbele katika vita dhidi ya mihadarati.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuhusu uhusiano wa kidugu baina ya mataifa mawili ya Iran na Jamhuri ya Azerbaijan.

Ilham Aliyev

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan naye akihutubu katika kikao hicho cha CIS kilichofanyika Ijumaa mjini Minsk, Belarus, amekanusha vikali madai hayo ya Aliyev  na kusema vyombo vya uslama vya Armenia na Iran vinashirikiana katika vita dhidi ya mihadarati.