Oct 18, 2021 11:26 UTC
  • Mohseni-Eje'i : Iran itawafuatilia na kuwatia adabu waliohusika na mauaji ya kigaidi ya Kamanda Soleimani

Mkuu wa Idara wa Mahakama nchini Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu itawafuatilia na kuwaadhibu wale wote waliohusika na mauaji ya kigaidi ya Kamanda Luteni Jenerali Qassem Soleimani.

Gholam-Hossein Mohseni-Eje'i ameashiria mauaji ya kigaidi yaliyofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Kamanda Qassem Soleimani na wanasayansi kadhaa wa Iran na kusema kuwa, wapngaji wa mauaji, waliotekeleza na walioshirika au kusaidia mauaji hayo kwa njia moja au nyingine wanapaswa kufuatilwia ipasavyo, na Tehran haitauhusu damu za wanadamu hao wasio na hatia zipotee bure. 

Amesema kuwa, Shetani Mkubwa (Marekani), Wazayuni na vibaraka wao wanaendelea kufanya jinai dhidi ya binadamu katika maeneo mbalimbali ya dunia na amewataka Waislamu kuwa macho na wasihadaiwe na njama za maadui hao za kutaka kuzusha mifarakano ndani ya Umma wa Kiislamu

Amesema wale wanaoituhumu Iran kuwa inakiuka haki za binadamu ndio wakiukaji wakubwa zaidi wa haki za binadamu duniani. 

Meja Jenerali, Qassim Solaimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH), aliuawa shahidi mwezi Januari mwaka jana katika shambulio la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mji mkuu wa Iraq.

Kamanda Soleimani

Kamanda Soleimani aliyekuwa safarini nchini Iraq kwa mwaliko wa waziri mkuu wa nchi hiyo, aliuawa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandes, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha al-Hashdul al-Shaabi,

Tags