Oct 20, 2021 07:21 UTC
  • Kasi ya chanjo nchini Iran yawashangaza Wamagharibi

Kasi kubwa ya zoezi la kudunga chanjo ya COVID-19 nchini Iran imezishangaza sana nchini za Magharibi.

Hayo yamedokezwa na Waziri wa Afya wa Iran Barham Einollahi ambaye ameongeza ku,wa maadui daima wamekuwa wakijaribu kuibua hitilafu baina ya wafanyakazi wa sekta ya afya Iran na wananchi lakini hawakufanikiwa.

Ameongeza kuwa, hivi sasa Iran imefanikiwa kutoa jumla ya chanjo milioni 75 za COVID-19 na kasi ya utoaji chanjo hizo imewashangaza sana Wamagharibi.

Ameongeza kuwa wiki iliyopita Iran ilifanikiwa kudunga jumla ya chanjo milioni 8.4 na idadi hiyo ni sawa na watu wote wa Umoja wa Falme za Kiarabu au  watu wote wa Kuwait na Qatar. Amesema nchi hizo zilichukua miezi kadhaa kuwadunga chanjo raa wake wote.

Chanjo ya Barkat iliyotengenezwa kikamilifu nchini Iran ni miongoni mwa chanjo ambazo zinatumika nchini kufanikisha zoezi la chanjo

Kwa ujumla nchini Iran hadi sasa watu 49,374,208 wamepokea dozi ya kwanza ya chanjo ya COVID-19  huku wengine milioni  26,006,109 wakiwa wamepokea dozi zote mbili  na kwa msingi huo  idadi ya chanjo zote ambazo zimedungwa nchini Iran ni millioni 75,380,317 hadi kufikia jana Jumanne.

Idadi ya watu nchini Iran ni milioni 83 na inatarajiwa kuwa wote watapata chanjo katika kipindi cha wiki chache zijazo. Hivi sasa serikali inatekeleza mkakati maalumu wa kuhakikisha kuwa wale ambao wamekuwa wakikataa chanjo wanashawishiwa kudungwa.