Oct 22, 2021 10:15 UTC
  • Gallop: Asilimia 72 ya watu wa Iran wanaridhishwa na utendaji wa serikali ya Raisi

Kwa mujibu wa takwimu za karibuni za matokeo ya uchunguzi wa maoni, asilimia 72 ya wananchi wa Iran wanaridhishwa na utendahi wa serikali ya Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wanaiunga mkono kikamilifu.

Gallop yenye makao makuu yake mjini Washington Marekani, imetoa matokeo ya uchunguzi uliofanyika karibuni kuhusiana na suala hilo na kusema kwamba kati ya watu wazima 10 nchini Iran zaidi ya saba kati yao wanaridhishwa na kuunga mkono utendaji wa serikali ya Raisi.

Takwimu hizo zilizochapishwa na shirika la Gallop ni kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanyika kati ya tarehe 24 hadi 31 za mwezi Agosti uliopita ikiwa ni wiki tatu baada ya kuingia madarakani Rais Ebrahim Raisi.

Wahudumu wa afya Iran

Shirika la Gallop pia limeashiria utendahi wa serikali ya Raisi kuhusiana na suala zima la utoaji chanjo ya kukabiliana na virusi vya corona na kusema kabla ya kuchaguliwa kuwa rais mwezi Juni, ni karibu asilimia tano tu ya Wairani ndio waliokuwa wamechanjwa lakini tokea wakati huo hadi sasa kiwango hicho kimeongezeka pakubwa na kufikia zaidi ya asilimia 50.

Shirika la Gallop ambalo ni shirika la ushauri kuhusu uongozi bora ni moja ya mashirika yenye itibari kubwa zaidi dunia katika uwanja wa uchunguzi wa maoni.