Oct 24, 2021 15:13 UTC
  • Iran iko tayari kushirikiana na nchi za Kiislamu katika uga wa nyuklia

Msemaji wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran (AEOI) amesema Jamhuri ya Kiislamu ipo tayari kushirikiana na nchi za Kiislamu katika sekta ya nishati ya nyuklia.

Behrouz Kamalvandi amesema hayo kwa mnasaba wa maadhimisho na sherehe za Maulidi ya Mtume Muhammad (SAW) na kuongeza kuwa: Tupo tayari kushirikiana na ulimwengu wa Kiislamu katika ustawishaji wa teknolojia ya nishati ya nyuklia kwa maslahi ya jamii za Waislamu, ili kuandaa mazingira ya ustaarabu mpya wa Kiislamu.

Sanjari na kuwapongeza wansayansi wa Kiislamu kwa mchango wao wa kupiga jeki maarifa na sayansi duniani, Kamalvandi ametoa mwito kwa jamii za Waislamu kuhuisha ustaarabu wa Kiislamu kupitia mwamko mpya. 

Kituoa cha nyuklia cha Fordow cha Iran

Kadhalika Msemaji wa Shirikia la Atomiki la Iran ametoa mwito kwa umma wa Kiislamu kuungana na kushirikiana mkabala wa mwenendo wa utumiaji mabavu na uchukuaji maamuzi wa upande mmoja wa madola ya kibeberu na kiistikbari.

Kabla ya hapo, Makamu wa Rais ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran (AEOI) Mohammad Eslami alisema nchi zote duniani zina haki ya kustafidi na teknolojia ya nishati ya nyuklia, kama ilivyoanishwa kwenye Hati ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).  

 

Tags