Oct 27, 2021 13:58 UTC
  • Iran na EU zajadili namna ya kuondolewa vikwazo vyote haramu katika JCPOA

Ofisi ya uwakilishi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Ulaya imetangaza kuwa, kuondolewa vikwazo vyote haramu na visivyo vya kisheria ilivyoekewa Iran ndio ajenda kuu ya mazungumzo ya Brussels kati ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa na mratibu wa kamisheni ya pamoja ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Katika ujumbe ilioandika kwenye mtandao wa twitter, ofisi ya uwakilishi ya Iran katika EU imeashiria mazungumzo ya Ali Bagheri, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Enrique Mora mratibu wa kamisheni ya pamoja ya JCPOA na Naibu wa Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya na kueleza kwamba, "mazungumzo ya Iran na Umoja wa Ulaya yanayolenga kutekelezwa kikamilifu na kivitendo makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na pande zote husika, ikiwa ni pamoja na kuondolewa vikwazo vyote visivyo vya kisheria ilivyoekewa Iran, yameanza leo mjini Brussels".

Bagheri (kulia) na Mora

Kuhusiana na utayari wa Iran wa kufanya mazungumzo na pande zote katika JCPOA, ofisi ya uwakilishi ya Jamhuri ya Kiislamu katika Umoja wa Ulaya imesema: "Iran imesisitiza utayari wake wa kuzungumza na pande zote zinazoaminika ili kuweza kupata njia ya ufumbuzi kupitia meza ya mazungumzo."

Habari kutoka Brussels zinaeleza kuwa, Bagheri na Mora wamekutana katika kikao cha faragha, kilichofanyika leo asubuhi katika jengo la Umoja wa Ulaya.../

 

Tags