Nov 15, 2021 11:51 UTC
  • Mjumbe Maalumu wa Iran: Marekani inaunga mkono ISIS

Mjumbe Maalum wa Rais wa Iran katika masuala ya Afghanistan amesema Marekani ilipata pigo na kushindwa vibaya huko Afghanistan, na sasa inajaribu kuliunga mkono kundi la kigaidi la Daesh (ISIS).

Hassan Kazemi Qomi amesema hayo leo Jumatatu baada ya kuwasili mjini Kabul na kuongeza kuwa, "nchi vamizi ambayo iliitawala Afghanistan kwa miaka 20 sasa inajaribu kuyapiga jeki makundi ya kitakfiri baada ya kushindwa."

Qomi ameeleza bayana kuwa, lengo la safari yake nchini Afghanistan ni kufanya mazungumzo na maafisa wa kundi la Taliban linaloongoza hivi sasa nchini humo kuhusu serikali ya mpito ya nchi hiyo, masuala ya kisiasa, kiuchumi, usalama na wakimbizi wa Kiafghani.

Mjumbe huyo maalumu wa Rais Ebrahim Raisi wa Iran amebainisha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inaheshimu azma na irada ya watu wa Afghanistan, na mtazamo wa serikali ya Tehran unaenda sambamba na mtazamo wa Waafghani.

Trump alipofichua kuwa US ndiyo iliyoasisi ISIS

Kadhalika Hassan Kazemi Qomi, Mjumbe Maalum wa Rais wa Iran katika masuala ya Afghanistan ameeleza matumaini yake kuwa, kwa kuundwa serikali thabiti nchini Afghanistan, uthabiti utashuhudiwa katika eneo.

Ameongeza kuwa, kama ilivyo kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jamhuri ya Afghanistan pia inakabiliwa na vikwazo vya kikatili vya Wamagharibi na kueleza kuwa, nchi mbili hizi zitafanya jitihada za kuboresha ushirikiano wa pande mbili na kuimarisha usalama katika mipaka yao. 

Tags