Nov 20, 2021 12:28 UTC
  • Mwanadiplomasia: Lengo la Marekani kuasisi makundi ya kigaidi ni kudhamini usalama wa Israel

Mwanadiplomasia wa zamani wa Iran amesema, lengo la Marekani la kuasisi makundi ya kigaidi katika eneo la Asia Magharibi hasa la DAESH (ISIS) ni kuvuruga uthabiti katika nchi zaWaislamu na kuzidhoofisha nchi zinazoupinga utawala wa Kizayuni kwa ajili ya kudhamini usalama wa utawala huo.

Mohsen Pak Aain ameliambia shirika la habari la IRNA kuhusu malengo ya madola ya nje ya eneo hili kuanzisha makundi ya kigaidi ya ukufurishaji katika miaka ya karibuni ya kwamba, Marekani inaamini kuwa kudhamini usalama wa utawala wa Kizayuni ni miongoni mwa mikakati yake ya kistratejia; na kutokana na kuondoka askari wake katika nchi za kanda hii, imefanya kila njia kuanzisha makundi ya kigaidi ili yafanye kazi na kwa niaba yake na kufanikisha malengo yake katika nchi za Asia Magharibi, ikiwemo Syria na Iraq.

Pak Aain amebainisha kuwa, lengo la Marekani, nchi za Ulaya na tawala zenye fikra mgando za eneo hili, lilikuwa ni kutoa mashinikizo kupitia kundi la Daesh ili kuipindua serikali halali ya rais Bashar al-Assad nchini Syria; na badala yake kuileta madarakani serikali inayofuata mitazamo ya Marekani; na sambamba na hilo zilitaka pia kuigawanya ardhi ya Syria mapande kadhaa.

Wanamgambo wa kundi la kigaidi la DAESH(ISIS) nchiniSyria

Mtaalamu huyo wa masuala ya kimataifa ameongeza kuwa, Wamarekani walifanya juu chini ili waweze kuigawanya Iraq katika mapande matatu ya Mashia, Wakurdi na Masuni; na kwa njia hiyo kuzidhoofisha nchi mbili za Waislamu zenye nguvu katika eneo, yaani Iraq na Syria ambazo zina mtazamo ulio dhidi ya Uzayuni na hivyo kuzitoa nje ya mduara wa mapambano dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.../

Tags