Nov 25, 2021 04:35 UTC
  • Iran yapinga madai yasiyo na msingi ya Bahrain

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametoa jibu kwa tamko la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain na kusema, madai yoyote ya wakuu wa Manama kuhusu kugundua silaha na mada za milipuko zinazohusishwa na Iran hayakubaliki.

Akizungumza Jumatano, Saeed Khatibzadeh, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amebaini kuwa, "madai kama hayo yasiyo na msingi yametolewa na watawala wa Bahrain sambamba na kufanyika kikao cha 'Mazungumzo ya Manama', ambacho kiligeuka na kuwa jukwaa la matamshi dhidi ya Iran, na jambo hilo linaonyesha Bahrain haidikiriki vyema masuala ya eneo.

Khatibzadeh ameongeza kuwa, serikali ya Bahrain inafadhilisha kuwa na uhusiano na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel badala ya uhusiano na wananchi wake na inajuzuia kutekeleza matakwa yao ya kiraia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameendelea kusema kuwa, serikali ya Bahrain haiwezi kuficha kushindwa kwake kutatua matatizo ya ndani ya nchi kwa kutoa matamshi kama hayo.

Idara ya Upelelezi wa Jinai ambayo inafungamana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain imedai kuwa imewakamata 'watu wanaohusishwa na ugaidi na kusambaratisha njama ya hujuma ya kigaidi' na ikaendelea kudai kuwa eti watu hao wana uhusiano na Iran.

Tags